Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amewaonya watumishi wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) mikoani na wilayani kutojihusisha na masuala ya Rushwa wakati wote wa kutimiza majukumu yao na kutoa onyo kwa watakaojihusisha watachukuliwa hatua kali zikiwemo kufukuzwa kazi.
Waziri Jafo amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya Maafisa wa TARURA wa Mikoa ya Kanda inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, simiyu, Geita, Kagera, Kigoma, na Tabora uliofanyika jijini Mwanza.
Waziri Jafo amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya Maafisa wa TARURA wa Mikoa ya Kanda inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, simiyu, Geita, Kagera, Kigoma, na Tabora uliofanyika jijini Mwanza.
Jafo amesisitiza kuwa serikali haitamvumilia mtumishi yoyote wa TARURA ambaye atafanya ubadhilifu wa aina yoyote kwenye miradi ya barabara na kusababisha miradi hiyo kukwana na kuwa chini ya kiwango.
Katika mafunzo hayo,washiriki wa mafunzo hayo wamejengewa uwezo katika swala la manunuzi, mikataba, maadili, Rushwa, Jinsia, Ukimwi, pamoja na afya na usalama mahala pa kazi.
Aidha mafunzo kama haya yamesha kamilika katika kanda zingine za kaskazini, na kanda mashariki na Kati na yanatarajiwa kukamilishwa kwa mikoa iliyobaki ya kanda za juu kusini mwanzoni mwa mwezi Januari 2018.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maafisa Tarura. |
No comments:
Write comments