Saturday, December 23, 2017
Mkurugenzi Arusha Dc anawatakia wananchi wote Heri ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya 2018
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru Dkt. Wilson Mahera Charles anawatakia wananchi wote na wakazi wa Halmashauri yake heri ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya wa 2018.
Aidha Dkt. Mahera amewataka wananchi wote kuwa watulivu katika kipindi chote cha sikukuu hizo na kuwasihi kusheherekea kwa amani na utulivu.
Ameongeza kwa kuwakumbusha wazazi na walezi kuwa makini katika uangalizi wa watoto na kuacha tabia ya kuwaruhusu watoto kwenda kutembea peke yao bila uangalizi wa watu wazima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments