Timu ya Young African ya Jijini Dar es Salaam inatarajia kukipiga na timu ya Njombe FC ya Njombe timu iliyopanda daraja katika msimu huu wa ligi, mechi itakayochezwa Mjini Njombe.
Yanga kama itaibuka na ushindi katika mechi yake dhidi ya Njombe FC ina uhakika wa kuifikia Simba kwa pointi.
Pamoja na kwamba Yanga iko ugenini, ina nafasi hiyo kama itapata pointi tatu kwa kuwa tayari ina moja baada ya kuanza na sare dhidi ya Lipuli FC.
Simba iliyoanza kwa kishindo cha mabao 7-0 dhidi ya Lipuli FC, jana ilikwama dhidi ya Azam FC baada ya kupata sare ya 0-0 ikiwa ugenini Chamazi.
Kama Yanga itashinda na kufikisha pointi 4 kama ilivyo kwa Simba, maana yake rasmi vita ya ubingwa itakuwa imeanza kwa kila upande na itachangia ligi hiyo kuamka.
Simba itakuwa inajivunia akaunti nzuri ya mabao lakini itakuwa na hofu katika pointi. Hivyo mashabiki wengi wa Simba watakuwa wakiomba Yanga ipoteze ili kutengeneza ahueni kwao.
Hata hivyo, Yanga wanalazimika kufanya kazi ya ziada kwa kuwa Njombe iliyopanda daraja inaonekana imejipanga kufanya vema.
Mechi hiyo mjini Njombe ndiyo itakayotupiwa macho na watu wengi zaidi ili kujua Yanga inaifikia Simba na kuanza mbio za kutetea ubingwa wake.
No comments:
Write comments