Tuesday, September 5, 2017
Wanafunzi 7676 wa darasa la saba kufanya mtihani kesho
Jumla ya wanafunzi 7676 wa darasa la saba katika shule za Msingi 116 za Halmashauri ya Arusha wamatarajia kufanya Mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka 2017.
Kati ya hao wanafunzi 4118 ni wasichana na wanafunzi 3558 ni wavulana ambapo shule 91 watafanya Mtihani kwa lugha ya Kiswahili na shule 25 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiingereza.
Mitihani hiyo itafanyika siku mbili tarehe 06-07/09/2017 kwa kufuata ratiba iliyoandaliwa na Baraza la Mtihani la Taifa.
Tunawatakia kila la Kheri wanafunzi wote wa darasa la saba waweze kufanya vizuri!
Ee Mwenyenzi Mungu wasimamie watoto hawa!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments