Tuesday, September 19, 2017

Serikali yajipanga kuboresha huduma ya umeme Kigamboni


Serikali imeahidi kukamilisha haraka miradi ya umeme kwenye kituo cha Tipper Kigamboni, Mbagala na Kurasini ili wananchi waondokane na kero ya kukosa huduma hiyo muhimu.

Hayo yamethibitishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani Septemba 18 wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua uboreshaji wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na kituo kipya cha kufua na kusambaza umeme wilayani Kigamboni.

Naibu Waziri huyo hakuishia hapo amefanya ukaguzi pia katika mradi wa maendeleo wa upanuzi na upatikanaji nishati (TEDAP) utakao safirisha 132kv za umeme uliopo Gongolamboto.

Waziri Kalemani amewataka wakandarasi kufanya kazi masaa 24 ili wakamilishe mradi huo kwa wakati kwani wananchi wanataka huduma ya umeme kwa wakati.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo