Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera amefungua mafunzo ya siku nne ya Mfumo wa kuandaa bajeti wa PLANREP kwa wataalamu wa Halmashauri ya Arusha yanayofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mafunzo hayo yamejumuisha wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Maafisa Bajeti kutoka kwenye Idara na Vitengo ambao kwa pamoja watajihusisha na utaratibu mzima wa uandaaji wa bajeti ya Halmashauri kwenye maeneo yao kulingana na shughuli zitakazofanyika na mfumo mzima wa matumizi kulingana na bajeti zao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Dkt. Mahera amewataka watumishi hao kuzingatia mafunzo hayo kwa kuwa mpango wa bajeti ndio dira ya shughuli zitakazotekelezwa ndani ya Halmashauri kwa mwaka mzima.
Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa kushindwa kupanga ni dhahiri itasababisha kushindwa kutekeleza shughuli za Halmashauri hivyo kila mtu kwa nafasi yake analazimika kuongeza umakini katika kujifunza ili kuwa na mpango mzuri wa mpango wa bajeti kwa mwaka ujao.
" Bajeti ni mpango hivyo kushindwa kupanga malengo itapelekea kushindwa kutekeleza malengo, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake awe makini kujifunga ili tupange mipango itakayotekelezeka kwenye bajeti yetu" amesisitiza Mkurugenzi huyo
Naye Mchumi wa Halmashauri ya Arusha Nhojo Kushoka amesema kuwa mfumo wa PLANREP ni mfumo mahususi wa kuandalia bajeti na kuwa si mfumo mpya kwa serikali za mitaa bali kwa sasa umeboreshwa zaidi kwa ajili ya kuongeza uwazi na udhibiti matumizi sahihi kilingana na mapato pamoja na malengo ya mpango wa bajeti ulioandalliwa.
Kushoka ameendelea kueleza kuwa mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo watumishi juu ya Mfumo wa PLANREP ambao umeboreshwa uliounganisha matawi ya mifumo mingine na kuunganishwa kwenye mfumo mmoja.
Aidha Kushoka amefafanua kuwa licha ya mfumo huo kuunganisha mifumo mingine pamoja Mfumo huu pia umeongeza uwanda wa uandaaji wa mpango wa bajeti kutoka Idara ya Mipango mpaka kwa wamiliki halisi wa bajeti ambao ni Idara na Vitengo na hakutakuwa na mwingiliano wa bajeti katika matumizi.
"Zamani Idara ya Mipango ilikua ikijikita zaidi katika uaandaaji na uingizaji wa shughuli na mipango ya matumizi lakini mfumo huu unamtaka user mwenyewe kuandaa mpango wa bajeti yake na shughuli zake za mwaka mzima pamoja na kucontrol matumizi" amesema Kushoka
Hata hivyo Kushoka amesema kuwa mfumo huu umepunguza gharama kwa kuwa maandalizi yatafanyika kwenye mfumo yaani on line kadhalika na uwalishaji wake tofauti na zamamani ilikuwa lazima watu kusafiri kwenda kuwasilisha bajeti hali ambayo kwa sasa haitakuwepo.
Picha za Matukio wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
No comments:
Write comments