Saturday, September 2, 2017

Halmashauri ya Arusha kupokea Mwenge wa Uhuru kesho 03.09.2017


Halmashauri ya Wilaya ya Arusha inategemea kupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 kesho tarehe 03.09.2017  wenye Kauli  ya  ”Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya nchi Yetu’. 


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti atakabidhiwa Mwenge wa Uhuru 2017 na Mkuu wa Wilaya ya Longido mnamo saa 02:00 asubhui katika eneo la Ofisi za Kata ya Oldonyowas na kuukimbiza katika Halmashauri ya Arusha.

Katika halmashuri ya Arusha Mwenge wa Uhuru  2017 utakimbizwa umbali wa Kilomita 88 katika kata 7 na kupitia jumla ya Miradi 7 iliyogusa sekta za Elimu, Afya, Maji, Viwanda na  Uvuvi yenye thamani ya Tsh. 1,635,900,399.45 fedha hizo zimetokana na vyanzo mbalimbali ikiwa kiasi cha Tsh.163,350,700.00 ni Nguvu za wananchi, Tsh. 80,849,699.45 Mapato ya Ndani ya Halmashauri,fedha kutoka Serikalini kiasi cha Tsh. 255,000,000.00 pamoja na Michango ya Wadau wa Maendeleo Tsh. 1,136,700,000.00.

Mwenge wa Uhuru 2017 utakimbizwa na kufanya shughuli za kuweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Tanki la Maji Ekenywa  kata ya Olturumet lenye Ujazo wa Mita 60 sawa na lita 60,000 mradi uliogharimu  kiasi cha shilingi 58,448,099.45, Kuzindua mradi wa Bweni la wasichana shule ya Sekondari Mwandet kata ya Mwandet  wenye thamni ya Tsh. 174,298,200.00, kuzindua ujenzi wa vyumba Vinne vya Madarasa ya kidato cha tano na sita shule ya Sekondari Mwendet kata ya Mwandet wenye thamani ya Tsh. 88,552,500.00.

Aidha Mwenge wa Uhuru 2017 utafungua Kituo cha Afya Engorora kata ya Kisongo wenye thamani ya Tsh. 151,501,600.00, kuzindua Kiwanda cha kutengeneza Vifungashio (maboksi) cha ’Active Packaging’ kijiji cha Loovlukuny kata ya Kisongo wenye thamani ya Tsh. 950,000,000.00’ kufungua mradi wa Mabwawa mawili ya kufugia Samaki kwenye Shamba la  ’Trust St. Patrick’ kata ya Olorien yenye uwezo wa kubeba samaki 8,000 wenye thamani ya Tsh. 83,000,000.00 pamoja na kuzindua Mradi wa Kivuko cha Moivo kinachounganisha kata za Moivo na Olturoto wenye thamani ya Tsh. 34,400,000.00.

Hata hivyo pamoja na kupitia Miradi ya Maendeleo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 kitaifa Ndugu Amour Hamad Amour atakabidhi Hundi za Mikopo zenye thamani ya Tsh. 100,000,000.00 kwa Vikundi 23, Vikundi 16 ni vya Wanawake na vikundi 7 vya Vijana.

Fedha hizo ni utekelezaji wa Sera ya Serikali ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya wanawake na vijana kwa kuwakopesha fedha kutokana na Mapato ya ndani kwa kiasi cha asilimia 10%, shughuli ambayo itafanyika kwenye eneo la Mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2017 katika Viwanja vya Ofisi za Makao Makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Arusha eneo la Sekei.

Baada ya kukabidhi Hundi hizo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti atasoma Risala ya Utii kwa Mheshimwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na baadaye kuendelea na shughuli nyingine.

Baada ya zoezi hilo, sherehe za mkesha wa Mwenge  wa Uhuru 2017 zitaanza na kuendelea mpaka asubuhi tarehe 04/09/2017 , saa 08:00 asubuhi Mwenge wa Uhuru 2017 utakabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru katika eneo la Soko la Tengeru.


No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo