Friday, August 4, 2017

Uhamiaji watahadharisha matumizi ya passport kama kitambulisho

IDARA ya Uhamiaji nchini imewataadharisha watanzania kuacha kutumia Passport kama kitambulisho kwa kuwa huo sio utaratibu.

Idara hiyo imewataka wananchi kutambua kuwa paspoti siyo kitambulisho ndani ya nchi na kwamba kisitumike kwa matumizi hayo kwa sababu siyo utaratibu uliopangwa kisheria ndani ya mipaka ya nchi.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Uhamiaji-Pasi na Uraia Gerald Kihinga alipozungumza na mwandishi wa habari kuwa hati yaa kusafiris hairuhusiwi kutumika kama kitambulisho ndani ya nchi na kuwataka wananchi kuacha mara moja kutumia kwa kuwa kinyume cha sheria ndani ya mipaka ya nchi.

Aidha amewataka wananchi kutambua kuwa passport zinazotolewa nchini zinapaswa kutunzwa na kutumika kwa lengo lililokusudiwa la kusafiria nje ya nchi na si vinginevyo na kuwq hati hizo hutumika kama kitambulisho wawapo nje ya nchi tu.

"Ninaomba mfahamu kuea passport zinazotolewa siyo vitambulisho ndani ya nchi hivyo visitumike kama vitambulisho ndani ya nchi na si vema kutembea nayo kila mahali kama huna safari ya nje ya nchi" amesisistiza Kamishna huyo.


Hata hivyo Kamishina Kihinga amesema kuwa kitambulisho rasmi cha Mtanzania anavhotakiwa kutembea nacho na kukitumia akiwa ndani ya nchi ni kile kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA.


Kamishna Kihinga amefafanua kuwa endapo itabainika mwanachi amepoteza hati hiyo ya kusafiria kwa uzembe hatapewa nyingine hivyo ni jukumu la kila mtu kutunza hati hiyo.

Ametoa tahadhari hiyo kutokana na kuwa na maombi mengi ya kutengeneza hati ya kusafiria ikiwa wengi wa wombaji hao kuwa na sababu ambazo kimsingi zinaashiria hakuna umakini wa mtu katika utunzaji wa hati hizo.

" Ninaomba mfahamu kuwa passport pia zinazotolewa siyo vitambulisho ndani ya nchi hivyo visitumike kama vitambulisho na tena si vizuri kutembea nayo kila mahali kama huna safari ya nje ya nchi.

Kamishna huyo pia amewataka wananchi raia wa Tanzania kutambua kuwa hati za kusafiria ni haki ya kila raia wa Tanzania na kuwa hati hizo zinaweza kupatikana popote Tanzania na kwa muda mfupi.


No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo