Tuesday, July 25, 2017

Arusha DC watambulisha mradi wa maji kwa jamii


Watalamu wa halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na wataalamu Washauri wa Don Consult Ltd wamefanya Mkutano na viongozi wa serikali, wazee wa mila na koo, watu mashuhuri wa kitongoji cha Ngaramtoni kata ya Olmotony kwa ajili ya kuutambulisha mradi wa maji utakaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la WaterAid mradi unaoanza Julai 2017 mpaka Mei 2018. Akitambulisha mradi huo mhandisi wa maji halmashauri ya Arusha mhandisi Joyce Bahati amesema kuwa halmashauri ya Arusha inategemea kuanza mradi mkubwa wa maji unaotegemea kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja kuanzia Julai 2017 mpaka Mei 2018 kwenye vijiji na vitongoji vitano Ngaramtoni ikiwepo. Mhandisi Bahati amefafanua kuwa mradi huu wa maji utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.5 utakao hudumia takribani watu 50,000 katika maeneo hayo na unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa Maendeleo DFID na kutekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la kimataifa WaterAid kwa kushirikiana na halmashauri ya Arusha. Hata hivyo wakati wa mkutano huo Mtaalam wa Masuala ya kijamii wa kampuni ya DON CONSULT Ltd Suzan Wagur amewaelezea viongozi hao na wawakilishi wa wananchi kutambua kwanza mradi huo ni wao hivyo ni lazima jamii kufahamu umuhimu wa maji katika jamii, utunzaji wa mazingira ya vyanzo vya maji, usafi wa mazingira na usafi wa maji pamoja na ujenzi wa vyoo bora katika kaya zao. Aidha Susaz alielezea kuwa mradi huo utawalazimu wananchi kugharamia maji hayo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa kulipia kabla ya kutumia 'eWater paid' ni vema kuwaeleza wananchi kufahamu uchangiaji wa huduma hiyo na kuwa uchangiaji huo utawezesha mradi kujiendesha na kudumu kwa muda mrefu. Afisa Mazingira halmashauri ya Arusha ndugu Ndelekwa Vanika amesema kuwa Jamii inapaswa kutambua kuwa mradi huu wa maji utaenda sambamba na utunzaji wa mazingira na ujenzi wa vyoo vya mfano hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutunza vyanzo vya maji kutokana na ukweli kwamba vyanzo vya maji vimepungua kutokana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya ta ia nchi. Diwani wa kata ya Olmotony mheshimiwa John Slim ameelezea matatizo ya maji katika eneo la Ngaramtoni na kuthibitisha kuwa mara nyingi ugonjwa wa kipindupindu huanzia Ngaramtoni kutokana na uhaba wa maji unaosababisha kutumia maji yasiyo safi wala salama. "Watu wa Ngaramtoni wanashida ya maji wananunua maji kwa gharama kubwa shilingi 500 mpaka 700 kwa ndoo na wasiyojua yanatoka wapi jambo ambalo husababisha kutumia maji yaliyotoka kwenye vyanzo visivyo salama" amefafanua Diwani huyo Pichani ni matukio ya mkutano huo Hata hivyo viongozi hao na wawakilishi wa wananchi wamekubali kuupokea mradi huo kwa kuwa katika eneo la Ngaramtoni kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kutokana na kukua kwa kasi kwa mji huo jambo linalosababisha shida ya maji na kulazimika kununua maji kutoka maeneo wasiyoyafahamu na kuahidi kushiriki kwa hali na mali ili kutimiza adhma ya serikali ya kuwapatia wananchi maji.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo