Wednesday, July 12, 2017

Wajumbe wa Kamati ya Fedha halmashauri ya Arusha waridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo




Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango halmashauri ya Arusha wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Noah Lembrisi wametembelea jumla ya miradi 27 katika kata 14 kati ya kata 27 za halamshauri ya Arusha.

Wajumbe hao wa Kamati ya Fedha wameendelea kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017na kusema kuwa hali ya miradi iliyotekelezwa mwaka huu fedha inaridhisha sana na imetekelezwa kwa wakati.

Wakizungumza wakati wa ziara hiyo wajumbe hao walionyesha kufurahishwa na shughuli zinazoendelea katika utekelezaji huo na kuwapongezwa wataalam wa halmashauri ya Arusha kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri kwa jitihada zao za kuhakikisha kazi zilizopangwa kufanyika katika miradi zinayotekelezwa kwa wakati na miradi hiyo inaonekana kwa macho kuwa gharama ya miradi inaendana na uhalisia wa mradi husika.

Kaimu Afisa Mipango Halmashauri ya Arusha ndugu Nhojo Kushoka ametaja miaradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Chumba cha Upasuaji Theater' kituo cha Afya Nduruma, ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya Msingi Majimoto, ukarabati wa vyumba vya madarasa shule ya Msingi Olomitu, ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya Zahanati ya Themiyasimba, Ujenzi wa choo cha wanafunzi shale ya Msingi Mungushi, Mradi wa maji Bwawani, ukarabati wa kituo cha Afya Mbuyuni-Oljoro,

Kushoka ameendelea kutaja miradi mingine ni Ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya Msingi Olemedeye, ujenzi wa shule mpya kata ya Laroi, ujenzi wa Kivuko cha kuunganisha wananchi wa Losinoni Juu na Losinoni Chekechea, ujenzi wa nyumba za walimu shule ya Msingi Namelok, ukarabati wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Oldonyosambu, Ukamilishaji wa nyumba ya walimu shule ya sekondari Oldonyosambu, Ujenzi wa Uzio mnada wa mifugo Oldonyosambu/Oldonyowas, ujenzi wa darasa shule ya Msingi Ilkonere, Ujenzi wa choo cha wanafunzi shale ya Sekondari Kiranyi, Ujenzi wa Chumba cha darasa shule ya Msingi Oldonyosapuk, Umaliziaji wa vyumba vya madarasa shule ya Msingi Olturoto na Ujenzi wa Kivuko Moivo kinachounganisha barabara ya Mahakamani ya mwanzo Enaboishu.




Jionee Picha za matukio ya ziara hiyo


Image may contain: 2 people, people standing and outdoorImage may contain: 3 people, people standing, sky, outdoor and nature



No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo