Wednesday, July 12, 2017

TAMISEMI wakagua Miradi ya Maendeleo halmashauri ya Arusha



Timu ya Wakaguzi kutoka Ofisi ya Rais za Mikoa na Serikali za Mitaa imefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Wakaguzi hao wamekagua jumla ya miradi saba kwenye kata za Moivo, Oltroto, Laroi, Kisongo na Musa.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja Ujenzi wa Daraja la Moivo linalounganisha Sanawari na Mahakama ya Enaboishu, Ujenzi wa choo Shule za Msingi Loruvani na Moivo, Ujenzi wa nyumba za walimu, choo na madarasa shule ya Sekondari Oljoro, Ujenzi wa kituo cha Afya wa Engorora, Ujenzi wa barabara Kisongo - Musa - Likamba - TPRI na pamoja Mradi wa Maji Likamba.































No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo