Madiwani wa kata 27 wasilisha taarifa za kata zao kwa kipindi cha robo ya nne ya kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2017 katika mkutano wa Baraza la Madiwa la Kata uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano halmashauri ya Arusha.
Mkuatano huo uliokuwa na agenda sita na agenda kuu ikiwa ni kuwasilsiha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya kata kwa robo ya nne ambayo ni robo ya mwisho kwa mwaka wa fedha ulioisha 2016/17.
Katika mkutano huo madiwani waliwasilisha taarifa mbalimbali za kata zao ikiwemo taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye kata zao, taarifa za fedha yaani mapato na matumizi, taarifa za Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Miundombinu ya barabara, Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii, hali ya chakula katika kata pamoja na taarifa za ulinzi na usalama.
Aidha Tarifaa zilizowasilishwa zilionyesha utekelezaji wa kasi wa miradi ya maendeleo iliyoanza kutekezwa mwaka wa fedha 2016/2017 huku baadhi ya miradi kuwa imekamilika kwa asilimia 100% na baadhi kufikia hatua za umaliziaji kwa kulingana na kiasi cha fedha kilichotengwa.
Hata hivyo changamoto kubwa iliyojitokeza kwenye taarifa zilizowasilishwa kwenye kata nyingi ni upungufu wa nyumba za kuishi walimu kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha ya fidia ya deni la Lakilaki zilipelekwa kwenye ujenzi na umaliziaji wa vyumba vya madarasa na vyoo vya wanafunzi.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mheshimiwa Godfrey Mashele ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo ameonyesha masikitiko yake juu ya adha wanayoipata walimu hasa wanaofundisha shule za pembezoni kwa kukosa nyumba za kuishi katika eneo la shule.
“Tumeshuhudia adha wanayoipa walimu hasa wanaofundisha shule za pembezoni kutokana na shule kukosa nyumba za kuishi walimu wetu jambo linaloashiria utendaji hafifu katika ufundishaji wa walimu hao, hivyo tunapaswa kuweka mikakati ziada katika shule hizo” amesema Makamu Mwenyekiti huyo
Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Arusha Dk. Wilson Mahera Charles ameahidi kuwa katika mwaka huu wa fedha 2017/18 kipaumbele cha halmashuri ni ujenzi wa nyumba za walimu zaidi ili kuwapunguzia adha ya kuishi mbali na shule.
“Walimu wanaofundisha shule za pembezoni wanapata kero kubwa ya mahali pa kuishi kutokana na shule hizo kutokuwa na nyumba za kuishi na baadhi ya maeneo hakuna nyumba za kupangisha, hivyo kipaumbele kikubwa katika mwaka huu mpya wa fedha ni ujenzi wa nyumba za walimu” amesisistiza Mahera
Mkutano wa Baraza la Madiwani la taarifa za kata huonesha taswira halisi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo za halmashauri na pia zinaiwezesha halmashauri kufanya tathmini ya hali halisi pamoja na kupanga mikakati thabiti ya kufikia malengo.
No comments:
Write comments