Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ametoa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka kwenye hospitali ya Mkomaindo iliyopo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kwa lengo la kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora za afya wawapo hospitali.
Rais Magufuli ametoa ametoa msaada wa vitanda 20, magodoro 20 pamoja na mashuka 5 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11 vifaa ambavyo vitapunguza tatizo la uhaba wa vifaa katika hozpitali hiyo ambayo ilikuwa inakabiliwa na changamoto hiyo.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Rais Magufuli, mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego amesema kuwa Rais Magufuli ametoa msaada huo wa vitanda,magodoro pamoja na mashuka ili wananchi wake wapate huduma bora za afya jitihada ambazo anazifanya nchi nzima.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Masasi Dk. Mussa Rashid ambae amepokea msaada huo amesema kuwa msaada huo umesaidi kupunguza tatizo la ukosefu wa vitanda vya kulaza wagonjwa katika hospitali ya Mkomaindo.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Masasi Dk. Mussa Rashid ambae amepokea msaada huo amesema kuwa msaada huo umesaidi kupunguza tatizo la ukosefu wa vitanda vya kulaza wagonjwa katika hospitali ya Mkomaindo.
" Hospitili ilikuwa na upungufu wa vitanda na kusababisha adha kwa wagonjwa wanaolazwa , msaada tuliopata umesaidia kupunguza tatizo hilo" amesisitiza Dk. Rashid
Aidha makabidhiano hayo yameenda sambamba na makabidhiano ya kadi za Bima ya Afya ya Jamii-CHF kwa wazee wa wa kata ya Temeke makabidhiano ambayo yamefanyika katika ujenzi wa zahanati ya kata ya Temeke inayokusudia kuondoa adha ya wakazi zaidi ya elfu kumi na moja wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
No comments:
Write comments