Tuesday, July 18, 2017

Mh. Baraka Simon Makamu Mwenyekiti mpya halmashauri ya Arusha


Na. Elinipa Lupembe.
Mheshimiwa Baraka Simoni Diwani wa kata ya Olturoto kwa tiketi ya  CHADEMA amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia sasa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha.
Mheshimiwa Baraka Simon amepata nafasi ya kuwa Makamu ya Mwenyekiti kwa kupata kura 27  kwa  kumshinda mpinzani wake mheshimiwa Yasmini Bachu diwani Viti Maalum CCM aliyepata kura 7 kati ya kura 34 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dk. Wilson Mahera amemtangaza mh. Baraka Simon kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri baada ya kushinda uchaguzi uliofanywa na wajumbe 34 wa Baraza la Madiwani waliohudhuria mkutano huo maalumu wa kumaliza mwaka wa fedha 2016/2017.
"Kwa mamlaka niliyopewa na Sheria za Serikali za mitaa sura ya 287 ninamtangaza mh.Baraka Simon kuwa makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha kwa muda wa mwaka mmoja" amesema Dk. Mahera
Hata hivyo mheshimiwa Baraka amewashukuru wajumbe wote wa baraza la madiwani kwa kumuamini na kumchagua kuwa Makamu Mwenyekiti na kuahidi ushirikiano kwa uongozi wa halmashauri kwa ujumla katika kuwatumikia wananchi.
Timu ya ARUSHADC NEWS BLOG inamtakia kila la kheri Mh. Baraka Simon katika kutekeleza majukumu mapya aliyokabidhiwa na wajumbe wa baraza la madiwani halmashauri ya Arusha.


No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo