Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha mheshimiwa Noah Lembris ameahidi kuhakikisha wananchi wa maeneo ya ambayo mradi wa maji unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la WaterAid kupata ajira za muda kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo.
Mheshimiwa Noah amesema hayo baada ya viongozi na wawakilishi wa wananchi kuomba vijana wao kupatiwa ajira za muda wakati wa utekelezaji wa mradi wa maji unaotekelezwa kuanzia mwezi Julai 2017 mpaka Mei 2017 katika vitongoji vya Ekenywa na Seuri kata Oltrumeti, kitongoji cha Ngaramtoni kata ya Olmotony, kijiji cha Olkokola kata ya Lemanyata na kijiji cha Lengijave kata ya Olkokola.
Viongozi hao walifikisha ombi lao wakati wa kikao cha pamoja cha viongozi na wawakilishi wa Kitongoji cha Ekenywa, wataalam wa halmashauri ya Arusha pamoja na wataalam wa Kampuni ya Don Consult amba ni wataalam washauri mradi waliokutana kwa lengo la kuutambilisha mradi huo wa maji kwa jamii, kikao kilichofanyika kwenye ofisi ya kitongoji cha Ekenywa kwa lengo la kuutambulisha mradi huo "Vijana wetu wengi wamesoma na wana vyeti lakini hawajapata ajira tunaomba vijana wetu wafaidi kwa kupata ajira kwenye hiyo kampuni itakayojenga mradi huo"alisema mwakilishi mmoja kwa niba ya wenzakke Mheshimiwa Noah amesema kuwa tutafanya mazungumzo na shirika la WaterAid ili wakati wa kusaini mkataba kuwatumia wananchi wa maeneo yote ambayo mradi huo utafanyika wapatiwe ajira za muda kulingana na kazi na kiwango cha elimu inayohitajika.
"Nimesikia ombi lenu mimi na mkurugenzi wa halmashauri tutashauriana kabla ya kusaini mkataba na kuuweka mazingira ya kutumia wananchi wa maeneo yetu kufanya kazi wakati wa utekelezaji, kwa kuhakikisha hilo suala hilo litaingizwa kwenye mkataba huo"amesisitiza Mwenyekiti Noah Aidha mheshimiwa Noah aliwataka viongozi hao kuwa mabalozi wa kuwaelimisha wananchi wao kuupokea mradi huo bila kukwamisha kwa lengo la kukamilisha mradi huo kwa wakati na kuondoa adha ya maji wanayoiata wananchi wa maeneo ya kata ya Oltumet na maeneo yote mradi huo unapotekelezwa.
Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Ekenywa mheshimiwa Joseph Tinayo licha ya wajumbe wote wa mkutano kukubali kwa psmoja kuupokea mradi na kutoa ushirikiano amethibitisha kuwa wananchi wa kitongoji cha Ekenywa ni wapenda maendeleo na endapo atatokea mkwamishaji hawatavumilia kutokana na adha ya maji inayowakabili wananchi wa Ekenywa.
" Niwahakikishie wananchi wa Ekenywa ni wapenda maendeleo hivyo niwathibitishie mimi na wananchi wangu kutoa ushirikiano wa hali na mali wakati wote wa utekelezaji wa mradi na kuwaelimisha wale watakao onyesha dalili ya kukwamisha mradi" amesisitiza Tinayo.
Mradi huo wa maji utatekelezwa kwenye kata nne, vitongoji vitatu vya Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni, vijiji viwili na unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la WaterAid kwa usimamizi wa halmashauri ya Arusha kwa ghara za takribabu shilingi bilioni 4.5.
No comments:
Write comments