Tuesday, July 18, 2017

Lifahamu jani hatari Gugu Karoti

Wajumbe wa baraza la madiwani wamepata fursa ya kuelimishwa juu ya jani la hatari linaloene kwa kasi katika mikoa ya Arusha, Manyara  na maeneo mengine nchini Tanzania.
Mafunzo hayo yametolewa na Bwana shamba wa shirika lisilo la kiserikali la la ECHO linalojishughulisha na usalama wa chakula na mazingira ndugu Charles Bonaventure ameeleza kuwa jani la Gugu Karoti limeenea sana katika maeneo ya mkoa wa Arusha na Manyara na hata katika maeneo ya halmashari hii ya Arusha.
Bwana Shamba huyo amefafanua kuwa tafiti zimeonyesha kuwa jani la Gugu Karoti lina madhara makubwa kwa binadamu, wanyama na mimea mingine hivyo ni jani hatari linalohitaji juhudi za ziada kuliangamiza.
Aidha ndugu Bonaventure amernda mbali zaidi na kufafanua Gugu Karoti lina madhara kwa binadamu ambapo akishika anaweza kuwashwa na kupata harara kwenye ngozi.
Aidha amefafanua kuwa ng'ombe akila jani hilo kwa asilimia 20% mpaka 50% mfululizo, ng'ombe huyo hufa na akichinjwa ini lake huwa ni gumu, majani hayo pia yakiota kwenye kingo za mito watu watakaotumia maji hayo hupata madhara pia.




Naye Daktari mkuu wa halmashauri ya Arusha amethibitisha uwepo wa jani hilo na madhara yake kwa binadamu na kusema kuwa binadamu anaposhika husababisha muwasho kwenye ngozi na ngozi kubabuka na moshi wa majani hayo husababisha athari kwenye mfumo wa hewa.
Hata hivyo ndugu Bonaventure ameitaka serikali na wadau wote kushiriki katika kuliangamiza janu hilo kwa kuling'oa na kulichoma kwa kuvaa gloves


No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo