Halmashauri ya Arusha imejipanga kufufua visima
vya maji ambavyo vimekamilika lakini havitoi
maji ingawa miradi hiyo ya maji imekamilika na kusababisha adha kubwa kwa
wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo visima hivyo havitoi maji.
Hayo yamethibitihswa na Mkurugenzi Mtendaji
halmashauri ya Arusha Dk. Wilson Mahera baada ya taarifa iliwasilishwa na
shirika la WaterAid ambao wanaotarajia kuanza kutekeleza mradi mkubwa wa maji
kwa mwaka wa fedha unaoanza 2017/2018 wenye thamani ya shilingi Bilioni 4.5
kwenye kata za Lemanyata, Olkokola na Oltrumet.
Akiwasilsisha ripoti ya utafiti wa awali kabla ya
kuanza kutekeleza mradi huo Mkurugenzi wa Mipango wa Shirika la WaterAid Abel
Dugange amesema kuwa tafiti zinaonyesha asilimia 75% ya vituo vya kuchotea maji
katika halmashauri ya Arusha havitoi maji licha ya miradi hiyo kukamilika kwa
muda sasa.
Dugange amesema kutokana na matokeo ya utafiti
huo WaterAid imejipanga kutekeleza mradi wa maji wenye matokeo endelevu kwa
kuhakiksha upatikanaji wa maji ya kutosha pamoja na miundo mbinu thabiti ya
ulipaji wa gharama za maji kulingana na mtumizi halisi ya mtumia maji.
Aidha Dugange amefafanua kuwa mradi huo unalenga
kutatua changamoto ya ukosefu wa maji
kwa kuwa umesanifiwa kwa kutumia teknolojia ya kulipia maji kabla ya kwa
kushirikiana na shirika la e-waterpay
pamoja na matumizi ya umeme wa nishati ya jua ‘solar’ jambo ambalo litasaidia
mradi huo kujiendesha mara baada ya kukamilika tofauti na miradi iliyotangulia.
Hata hivy Dk. Mahera amesema kuwa halmashauri
imejipanga kufufua vituo hivyo vya maji kwa kutumia fursa ya serikali kupitia
mkakati wa Wizara ya Maji wa lipa kutokana na matokeo ‘Payment by Results’.
Dk. Mahera ameulezea mkakati wa Wizara ya maji wa
lipa kutokana na matokeo ni unaelekeza kuwa unapofufua kituo kimoja cha kuchotea maji
unalipwa kiasi cha Paundi 1500 hali inayochochea kuhakikisha vituo hivyo vya
kuchotea maji vinafufuliwa ili kupata fedha hzio ambazo zitasaidia kufufua
karibu vituo vyote ambavyo havifanyi kazi.
“Mikakati
yetu ni kuhakikisha tunapata fedha za ‘payment for results’ kwa kufanya kazi kwa
weledi na utaalamu wa hali ya juu na kukamilisha kwa wakati kwa ajili ya
kuendelea kufufua vituo vya kuchotea maji ambavyo havifanyi kazi kwa sasa”
amesisitiza Mkurugenzi Mahera
No comments:
Write comments