Kwa watanzania wote wajengao,kuna mchezo mchafu unaofanyika katika viwanda vya mabati au wakala wao ambapo wauzaji na mafundi hushirikiana kwa pamoja kumwibia mteja kwa mbinu hii…, fundi anapopima vipimo vya mabati huwa wanakuwa na vipimo halisi (halali)na vingine feki(alizoongeza kwa kila pc ya bati) mara nyingi huongeza nusu mita(sentimita 50 hadi 70) hivyo anapokwenda kufanya manunuzi au kutoa oda kwenye viwanda ama wakala wa kiwanda huwa na karatasi mbili, ile feki yenye vipimo vilivyoongezwa ndio humpatia mwenye nyumba ambapo mara nyingi mafundi hao huwa wameshaongea na wahusika ktk katika kiwanda au wakala na humlazimisha mwenye nyumba kufanya manunuzi mahali alipokusudia kufanya uhalifu huo(uwizi)hivyo vipimo vilivyoongwezwa mita ndio hupigiwa mahesabu.
Mfano kwenye oda anapigiwa mahesabu ya mita 560 mara bei waliyopatana,hivyo mteja hulipia mita 560,baada ya mteja kuondoka,fundi huleta vipimo halisi. Mfano ni 480,hivyo ile tofauti basi hupigiwa hesabu mara bei na kugawana fedha hizo, ambapo kwakweli ukiangalia tofauti huwa ni kubwa sana huwa ni kati ya mita 70 hadi mita 120 kulingana na ukubwa wa nyumba,na bei kwa mita mara nyingi ni kati ya 12000 kwa mita hadi 11500 kwa mita.
Hivyo ukizidisha mara hizo mita,hujikuta fedha unazopoteza ni gharama za kumlipa fundi.
USHAURI: Kila mwenye kujenga ama mwenye kununua mabati haswa haya ya kukatwa kwa mita, hakikisha unakuwa na kopi ya vipimo ambayo fundi amekupa na unapokwenda kuchukua bidhaa yako hakikisha unapima kila pc kulingana na kopi uliyonayo. Hakikisha bati zisipigwe hadi uhakiki.
Tuma ujumbe huu kwa kila group umuokoe mtanzania mwenzako katika ubadhirifu huu unaofanywa na mafundi wengi wa kupaua nyumba wakishirikiana na wenye kuuza mabati kwa kisingizio eti "matajiri wanatubana kwenye malipo"
No comments:
Write comments