Halmashauri ya
Arusha imeadhimisha siku ya walemavu wa ngozi kwa kuwakutanisha pamoja watu wenye
ulemavu wa ngozi na kufanya mjadala juu ya haki na wajibu wao kwao wenyewe, kwa
jamii na kwa taifa kwa ujumla.
Mjadala huo uliendeshwa
na wao wenyewe kwa kuongozwa na mwenyekiti wa Chama cha walemavu wa ngozi mkoa wa
Arusha ndugu Edward Kivuyo ulilenga hasa kufahamiana na kufahamu haki na wajibu
wa watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na kutumia fursa zinazotelewa na serikali
kwa ajili yao.
NduguKivuyoamewasisitizanakuwakumbushawatuhaowenyeUalbinokuwaserikaliinatoafursanyingikwaajiliyaokazikubwawaliyonayonikuzitumiafursahizopamojanakuhakikishawanafuatasherianataratibuzanchikamaraiawenginewaTanznaia.
Aidha ndugu Kivuyo
amewasisistiza kudai haki baada ya kuwajibika na kutekeleza majukumu yao katika
kufanyakazi na kuachana na tabia ya kujilemaza
kutokana na ulemavu walionao kwa kuwa wanauwezo wa kufanyaa kazi kama watu wengine.
“Mtu mwenye ualbino
ana viungo vyote vya mwili hivyo hana shida yoyote katika kuwajibika na kufanya
kazi, mna uwezo mkubwa wa kufanyakazi hivyo ndugu zanguni naomba mfanyekazi kwa
kujituma ili msionekane kama ni mizigo kwenye jamii” amesisistiza Kivuyo
Naye Upendo Mollel
msichana mwenye ulemavu wa ngozi amewasisitiza wenzake kuwa licha ya changamoto
zinazowakabili si vizuri kukata tama na kubweteka kwa kuwa anaamini walemavu wa
ngozi wanauwezo mkubwa kuliko hata watu wasio na ulemavu.
Serikali ya ya
awamu ya tano imejitahidi kuhakikisha ulinzi na usalama wetu kwa hiyo tutumie fursa
hiyo tujiamini kama ni mwanafunzi soma kwa bidii utafanikiwa kuliko kuendelea kulalamika
kila siku, kwa kufanya hivyo unakuwa unajinyanyasa mwenyewe.
“Katika shule ya
sekondari niliyosoma wanafunzi wa kidato cha nne tulikuwa 17 wanafunzi wenye Ualbino tulikuwa 9 na wote tumefaulu
vizuri zaidi ya wenzetu wasio na ualbino, tumepata daraja la kwanza na la pili
na zaidi wote tumepangiwa shule za kidato cha tano, as long as umepata fursa na
sisi tunatakiwa kuzitumiz vizuri kwa tujitahidi hakuna mtu atakunyima ajira kama
una cheti kizuri kwa kigezo wewe ni Albino
haiwezekani “ alisistiza Upendo.
Katika maadhimisho
hayo Mkurugenzi Mtendaji halmashauriya Arusha Dk. Wilson Mahera aliwakabidhi mafuta
maalumu ya kupaka watu wenye ulemavu wa ngozi yenye thamani ya shilingi laki
sita fedha zilizotolewa na Halmashauri ya Arusha kama zawadi kwa ajili ya siku hiyo
maalumu kwa ajili ya walemavu hao.
Hata hivyo Mkurugezi
Mahera amewaahidi kuendelea kutoa ushirikoano wa hali na mali pale inapobidi na
kuahidi kuanzisha Kliniki ya ngozi katika hospitali ya wilaya ya Oltrumet kwa ajili
ya kutibiwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Maadhimisho ya siku
ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino hufanyika kila mwaka na kauili mbiu ya mwaka
huu ni Umuhimu wa Takwimu na Tafiti kwa watu wenye Ualbino kiwilaya, mkoa
,kitaifa na kiamtaifa.
No comments:
Write comments