Monday, November 13, 2017
Wanafunzi 6,506 wa kidato cha pili halmashauri ya Arusha wameanza mtihani wa taifa 2017
Jumla ya Wanafunzi 6,506 wa kidato cha pili katika shule 49 za sekondari wameanza mtihani wa taifa mwaka 2017 leo.
Afisa Vifaa na Takwimu Halmashauri ya Arusha Philip Mwakapalila amefafanua kuwa kati ya wanafunzi hao wasichana ni 3,489 na wavulana ni 3017 na jumla ya masomo 14 yatafanyiwa mitihani hiyo.
Ameongeza kuwa kati ya masomo kumi na nne, masomo 12 ni lazima kufanywa na wanafunzi wote na masomo mawili ni ya kuchagua 'option' ambayo ni masomo ya Biashara yaani Book Keeping na Commerce.
Mwakapalila amesema kuwa wanafunzi hao wameandaliwa vizuri kiakili na kisaikolojia hivyo wanategemea kupata matokeo mazuri ya ufaulu wa mitihani hiyo.
Uongozi wa halmashauri ya Arusha unawatakia kila la kheri katika mitihani yao waweze kufaulu na kuendelea na kidato cha tatu na hatimaye kutimiza ndoto zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments