Na. Elinipa Lupembe.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mashaka Gambo amewataka watumishi wa Halmashauri ya Arusha kufanya kazi kama timu na zaidi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mashaka Gambo amewataka watumishi wa Halmashauri ya Arusha kufanya kazi kama timu na zaidi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Mkuu wa mkoa Gambo amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Makao Makuu ya halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru kwenye Ukumbi wa Mikutano siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano iliyoanza leo katika halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.
Amesisitiza kuwa kila mtumishi anafahamu majukumu ya kazi yake, wajibu wake pamoja na mipaka ya kazi yake hivyo ni vema kila mtu akaheshimu majukumu ya kila mtumishi na kufanyakazi kwa pamoja kama timu.
"Ni vema kufanyakazi kwa ushirikiano kama familia moja,nasisitiza zaidi kuheshimiana katika eneo la kazi kwa kuzingatia vyeo na hata umri wa mtumishi mwenzio, pia ni utaratibu mzuri kukaa pamoja na kuzungumza pale inapotokea kutokuelewana kikazi na kupata suluhisho la tatizo na baadaye kazi ziendelee" amesisitiza
Aidha amewataka wataalam hao kutumia taaluma zao kufanyakazi kwa weledi na kwa kujiamini ili kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa maendeleo ya taifa letu la Tanzania.
Amesema kuwa licha ya watumishi kukatishwa tamaa na changamoto za kimaslahi kama kupandishwa madaraja, nyongeza za mishahara pamoja na marekebusho ya mishahara lakini niwahakikishie serikali iko katika mchakato ambao ukifika ukomo watumishi watalipwa madeni pamoja na stahiki zote.
" Niwaombe watumishi muwe wavumilivu kwa hili lakini zaidi kufanyakazi kwa kuweka mbele uzalendo kwa kuwa hakuna mtumishi anayedai stahiki yake ikapotea lazima serikali itawalipa" amessisitiza Gambo
Hata hivyo amewataka viongozi wa halmashauri ikiwemo wataalam na Baraza la Madiwan kujaribu kulipa madai madogo ya watumishi kwa kutumia mapato ya ndani na halmashauri ikabaki inaidai serikali.
Mkuu wa mkoa huyo ameendelea kumtaka kila mtumishi kuandaa mpango kazi wa wiki na kila mtumishi kufanya tathmini ya kazi za alizopanga kufanya pamoja na kutatua changamoto zinazokwamisha uhalisia wa utekelezaji wa changamoto hizo.
Sambamba na hilo Mkuu wa mkoa ameagiza watumishi wa idara ya Kilimo walioko ofisi za makao makuu kuhamia vijijini ambako ndio kuna wakulima wanaohitaji ushauri wa kilimo na kuagiza kuwa katika ofisi za makao makuu wabaki wataalam wasiozidi watatu kwa ajili ya shughuli za kiofisi.
Akizungumzia masuala ya viwanda mkuu wa mkoa ameutaka uongozi wa halmashauri kuweka mazingira rafiki kwa wananchi wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya viwanda kwa kuwaandalia mazingira yatakayopunguza kama si kuondoa ukiritimba ambao unawakatisha tamaa wawekezaji wengi wenye nia ya kuanzisha viwanda.

No comments:
Write comments