Tuesday, September 12, 2017

Mkuu wa Arusha atembelea Kijiji cha Watoto SOS na kuchangia shilingi milioni moja



Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mashaka Mrisho Gambo ametembeleza Kijiji cha Watoto cha SOS kinacholea watoto Yatima kilichopo eneo la Ngaramtoni katika Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru na kuzungumza na watoto na walezi wa  watoto hao.

Akiwa katika Kijiji hicho cha watoto SOS mkuu wa mkoa huyo amejionea makazi ya watoto hayo na kushuhudia namna kituo hicho kinavyotunza na kulea watoto yatima kimaadili na kwa kuwaweka makundi ya kuishi kama familia tofauti na vituo vingine .

Mheshimiwa Gambo amethibitisha utofauti mkubwa alioushuhudia wa malezi ya watoto hao tofauti ambayo ni  kubwa akilinganisha na vituo vingine  alivyowahi kujionea na kuthibitisha  kuwa kuna haja ya hata wazazi kufika eneo hilo kujifunza malezi bora ya watoto yanayotolewa katika kijiji hicho.

Gambo ameshuhudia mafanikio makubwa waliyoyapata watoto waliolelewa katika kijiji hicho baada ya baadhi ya watoto kueleza mafanikio yao mbele ya mkuu huyo wa mkoa wa Arusha.

"Nimeshuhudia kila mtoto ana stori ya mafanikio ambayo yanaonekana wazi jambo ambalo jamii inapaswa kujifunza kwa ajili ya malezi ya watoto hata wanaolelewa na wazazi" amesisitiza
Keriyombot Stephano kijana wa miaka 20 aliyehitimu masomo yake ya Stashahada ya Sayansi ya Komputa katika Biashara nchini Ghana amesema kuwa alikuja kwenye Kijiji cha SOS akiwa na umri wa miaka 2 na amelelewa kituoni hapo kwa upendo na kupewa mahitaji yote ambayo mtoto anapaswa kupewa ikiwa ni pamoja na kupelekwa shule.
"Nilikuja hapa nikiwa na miaka 2 na nimelelewa katika  maadili ya kitanzania, nimesomeshwa vizuri na sasa nimemaliza diploma ya Computer  Science in Business na nimefaulu nategemea kwenda kuanza masomo ya first  degree South Africa"

Keriyomboti amekiri kuwa malezi aliyoyapa kijijini hapo yamemuwezesha kujitambua na kujiamini jambo ambalo limemuwezesha sasa kujiunga na kikundi cha kuelimisha rika ambacho wanatembea kwenye shule na kueafundisha vijana stadi za maisha na masuala ya afya. 

Aidha mkuu wa mkoa ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Kijiji cha SOS na kuahidi  kuwaunga mkono kwa kufanya harambee kwa ajili ya kupata fedha za kutatua changamoto zinazokikabili Kijiji hicho.

Hata hivyo Gambo ameutaka uongozi wa Kijiji hicho kuandaa andiko kwa ajili ya kuongeza Green House nyingine inayotumiwa na wanafunzi hao kujifunza elimu ya kujitegeme pamoja na kupata chakul cha watoto wa kijiji hicho.

Awali mkurugenzi wa Kijiji cha SOS ndugu Francis Msoro amemueleza mkuu wa mkoa huyo kuwa kituo hicho kinalea jumla ya familia 15 zenye watoto 150 na familia za vijana 50 ambao hawana wazazi wote  wanaoishi kijijini hapo pamoja na watoto 1000 wanaoishi na mzazi mmoja katika familia zao.

Hata hivyo Msoro ameelezea kuwa licha ya mafanikio ya malezi bora ya watoto hao kwa sasa Kituo kinakabiliwa na changamoto ya fedha kutokana na baadhi ya wafadhili kutoka nje ya nchi kujiondoa kutokana na sababu mbali mbali za kiuchumi zinazokabili nchi zao.

Pichani ni picha za matukio yaliyojili katika Kijiji cha SOS












No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo