Sunday, September 17, 2017

Gambo afungua mradi wa TERRA unaojishughulisha na uchakataji wa ngozi



Mkuu wa mkoa wa Arusha Mashaka Mrisho Gambo amefungua mradi wa TERRA unaojishughulisha na kuchakata na kusindika ngozi na kutengeneza bidhaa za ngozi katika kijiji cha Uwira wilayani Arumeru.

Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika eneo la mradi huo mkuu wa mkoa  amesema kuwa amefurahishwa na uendeshaji wa shughuli zinazofanyika kiwandani hapo hasa katika matumizi ya raslimali za ngozi ambazo zinapatikana katika maeneo hayo ya wafugaji na zaidi unawanufaisha wananchi wa halmashauri za Arusha, Jiji la Arusha na Meru za mkoa wa Arusha.

Fursa hii ni muhimu kwa jamii ya Watanzani wafugaji kwa kuongeza thamani kwenye zao la mifugo yao kwa kutumia raslimali ya ngozi inayotokana na mifugo yao wenyewe na kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi na kuziuza ndani na nje ya nchi.

Awali balozi wa Italy nchini Tanzania Roberto Mengio amesema kuwa mradi wa TERRA licha ya kuwa na lengo la kuboresha maisha ya jamii ya wafugaji pia unakabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuhakikisha matumizi bora ya ardhi kwa kuboresha malisho na misitu ya asili.

Aidha balozi huyo amefafanua kuwa uzalishaji wa ngozi umeonekana ndiyo shughuli mbadala inayotoa fursa za kupata kipato endelevu kwa wananchi wa jamii ya wafugaji katika eneo hili la Kwiru.

Balozi Mengio mesema kuwa mradi wa TERRA uko umegharimu kiasi cha Bilioni 3 fedha zilizofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Italy (IADC) ambao utatekelezwa kwenye kata tatu na vijiji vitatu ndani ya halmashauri ya tatu za mkoa wa Arusha mradi utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

Hata hivyo mkuu wa mkoa alipata nafasi ya kupanda mti kama ishara ya ufunguzi na  wa mradi unaokwenda sambamba na utunzaji mazingira.

Janes Lucas mmoja wa mwanakikundi wanaofanya shughuli kiwandani hapo amethibitisha umuhimu wa kiwanda hicho kwao kama jamii ya wafugaji kwa kuwa uwepo wa kiwanda hicho umeongeza thamani kwenye ng'ombe wanaowafuga.

"Zamani tulikuwa tunajua zao la ng'ombe ni nyama na mazima lakini sasa hadi ngozi ni mali inayotupatia fedha kwa ajili ya familia zetu" amesema Janes

Picha za matukio ya shughuli za ufunguzi wa mradi wa TERRA.








No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo