Sunday, June 18, 2017

Majeruhi wa Lucky Vincent kurejea nchini Agosti

Watoto watatu walionusurika katika ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent ya mjini Arusha, huenda wakaruhusiwa kurejea nchini baada ya miezi miwili.
Taarifa hiyo imetolewa na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook.
Pia, Nyalandu ameandika katika mtandao huo kuwa watoto hao; Doreen Mshanga, Saidia Ismael na Wilson Tarimo wanategemewa kutembea tena.
Hata hivyo, kwa sasa Doreen, atahamishiwa katika kituo maalumu kwa ajili ya matibabu ya uti wa mgongo cha Madonna katika mji wa Lincoln, Nebraska.
Katika watoto wote hao watatu, Doreen ni muujiza mkubwa zaidi.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo