Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati wa kongamano na kufungua mwaka wa mafunzo kwa vijana liliofanyika jiji Dar es Salaam.
Profesa Ndalichako amesema kuwa anatamani kuona vijana wote nchinj wanakuwa na maadili mema na kuwa raia wema.
Ameongeza kuwa inawezekana jamii kushiriki kuwaandaa vijana kuwa na maadili mema na kuwataka vijana wenyewe kuwa tayari kupokea mafundisho kutoka kwa wazazi na walezi wao.
"Katika wadhifa wangu natamani kuona siku moja vijana wote nchini wanakuwa na maadili mema naaona hilo linawezekana iwapo kila mtu katika jamii atashiriki kuwandaa vijana kuwa raia wema na zaidi ni wajibu wa vijana wenyewe kuwa tayari kupokea mafundisho kutoka kwa walezi wao" amesema Waziri Ndalichako.
No comments:
Write comments