Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Waziri Jafo amesema wanafunzi hao waliochaguliwa kwa awamu ya kwanza ni sawa na asilimia 98.31 kati ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo na kuwataja wanafunzi wengine 11,173 sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakuweza kupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu hiyo kutokana na uhaba wa miundombinu.
Amesema idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu imeongezeka kwa jumla ya wanafunzi 124,209 likiwa ongezeko la asilimia 23.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka huu.
Aidha, amesema baadhi ya wanafunzi wa mikoa ya Lindi, Mbeya, Rukwa, Manyara, Katavi na Simiyu, wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu katika mikoa yao vikiwemo vyumba vya madarasa.
No comments:
Write comments