Saturday, December 9, 2017

Wananchi wa Kijiji cha Olkokola wanahitaji elimu zaidi ya umiliki wa vyanzo vya maji na uchangiaji gharama za maji


Wananchi wa Kijiji cha Olkokola wakijadiliana kwenye Mkutano wa kijiji juu mradi wa maji wa vijiji vitano maarufu kama WaterAid unaotekelezwa kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo ya Uingereza 'DFID' kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Kijiji cha Olkokola kata ya Lemanyata ni moja ya kijiji kilichpo kwenye mradi huo ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 4.5.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi hao wa kijiji cha Olkokola wanaonyesha kukataa kata kata  kupokea mradio huo wa maji kwa madai kuwa mradi huo umesanifiwa kutumia vyanzo vyao vya maji na kuwa wananchi hawana uwezo wa kulipia gharama za maji.

Tafiti zinaonyesha kuwa miradi mingi ya maji inashindwa kufanyakazi kutokana na kutokuwa na fedha za kuendesha miradi na kusababisga miradi kushindwa kutoa maji miaka michache tuu mara baada ya wafadhili kumaliza kutekeleza miradi.

Kwa kuliona hilo Serikali ikaona ni vema wananchi kuchangia huduma za maji ili miradi ya maji iweze kujiendesha na kuwa na huduma endelevu za maji.

Jambo la kusikitisha zaidi hata wanawake wa Olkokola wanaotumia muda mwingi kuchota maji wamekuwa mstari wa mbele kukataa mradi huo wa maji licha ya Kauli Mbinu na mipango ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya "MTUE MAMA NDOO" na lengo la kuhakikisha maji yanapatikana umbali usiozidi mita 400 na mwanamke.

Hata hivyo halmashauri imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hao juu ya umuhimu wa kuwa na MAJI SAFI NA SALAMA pamoja na Sera ya Serikali ya mwaka 2002 na sheria namba 12  ya mwaka 2009 ya kulipia huduna ya maji.

Aidha wananchi wanapaswa kufahamu kuwa Rasilimali maji ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulingana na Sheria namba 11 ya mwaka 2009 kifungu cha 10 hivyo mtu yoyote anaruhusiwa kutumia kwa mujibu wa sheria.

Kauli mbiu ya Wizara ya Maji na Umwagiliji  ya  MTUE MAMA NDOO ina lengo la kuhakikisha maji yanapatikana umbali usiozidi mita 400 kwa kila mwananchi.

Wananchi wote wanapaswa kuelewa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma zote za jamii ikiwemo Maji, Elimu, Afya na Miundo mbupinu ya barabara ndani ya maeneo yao.


PICHA ZA MATUKIO YA MKUTANO HUO. 














No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...