Kama ilivyokawaida ya wananchi wengi katika karne hii kuwa na shauku ya kupata maendeleo katika maeneo yao hata kwa kuchangia kiasi cha fedha, mali na hata nguvu zao ikiwa ni lengo moja kubwa la kuhakikisha huduma zote za jamii zinapatikana kwa urahisi katika maeneo wanayoishi.
Hali hiyo imejitokeza mubashara kwa wakazi wa Kitongoji cha Ekenywa kata ya Olturumet halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wakati wa mkutano mkuu wa kitongoji hicho kwenye viwanja vya shule ya Msingi Ekenywa na kukutana na Timu ya watalamu watekelezaji wa mradi wa maji wa vijiji vitano mradi unaotekelezwa na shirika la waterAid Tanzania kwa ufadhili wa Idara ya Maendeleo Uingereza 'DFID'
Wananchi hao wameonesha ari kubwa ya kutaka mradi huo uanze hata kesho kwa kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji katika eneo hilo na kusababisha wananchi hasa wanawake kutumia muda mrefu kutafuta maji jambo ambalo linapoteza muda wa kulijenga taifa na kuchelewesha maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Wananchi hao kwa pamoja wamesema kuwa wanahitiji maji kwa gharama yoyote na wako tayari kulipia maji kutokana na kupoteza muda mwingi kutafuta maji na wakati mwingine kuyakosa na kutumia maji yasiyo safi na salama kwa afya zao
Akizungumza wakati wa mkutano huo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ekenywa Joseph Tinayo amesema kuwa wakati umefika sasa wadau wa mradi kuanza kutekeleza mradi huo kwa kuwa wananchi wa Ekenywa wamechoka kuteseka na maji na wana hamu sasa ya kupata maji safi na salama.
Aidha ameongeza kuwa kutokana na adha kubwa ya maji wanayoipata wakazi wa Ekenywa wananchi hawatakubaliana na mtu yoyote anayefikiria kukwamisha mradi huo wa maji usiendelee na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huo.
Gabriel Elimwarabu mkazibwa Ekenywa amesema kuwa kwa kuwa Mungu amejibu maombi yao ya muda mrefu mradibuanze haraka ili kuwafuta machungu ya mateso wanayoyapata kutokana na uhaba wa maji na kuongeza kuwa wako tayari kitoa ushirikiano wa aina yoyote kwenye utekelezaji wa mradi huo
"Tunaamini Mungu amejibu maombi yetu ya muda mrefu Wanaekenywa, tuna machungu na maji leteni mradi sisi tutatoa ushirikiano wa hali na mali ilimradi tupate maji ya uhakika" amesema
Hata hivyo wananchi hao walilazimika kuchagua wajumbe 10 wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi wa mradi ambao watashiriki kwa zamu kusimamia hatua zote za utekelezaji wa mradi.
Wajumbe waliochaguliwa kwenye Kamati hiyo ni pamoja na Gabriel Lashilunye, Victor Gorovan, Paringo Juma, Ally Kimweli, Gasper Jonathani, Happy Ezekieli, Emanuel Elirehema na Joyce Sabaya.
Ekenywa ni moja kati ya vitongoji Vitatu na vijiji viwili amvavyo Mradi wa maji wa Vijiji vitano unatekelezwa kwa Ufadhili wa Idara ya Maendeleo Uingereza na kutekelezwa na Shirika la WaterAid -Tanzania kwa gharama ya shilingi bilioni 4.5 na unategemea kuhudumia takribani watu elfu hamsini.
PICHA ZA MATUKIO YA MKUTANO HUO
No comments:
Write comments