Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza kupitia Shirika la lisilo la Serikali NASIO TRUST CHANGING LIFES FOR GOOD la nchini Kenya wametoa msaada wa matanki ya maji kwa ajili ya kuvunia maji ya mvua kwa wananchi wa kijiji cha Lemanda kata ya Oldonyosambu.
Wanafunzi hao wametoa jumla ya matanki 8 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa wastani wa shilingi 625 kwa tanki lenye ujazo wa lita 3000 kwa wananchi walio kwenye hatari ya kuathirika na maji yenye madini ya Floraidi kwa lengo la kupambana na madini hayo.
Wanafunzi hao wakiwa na mwenyeji wao Diwani wa Kata ya Oldonyosambu mheshimiwa Raymond Lairumbe wamesema kuwa wamefarijika kufika eneo la Lemanda na kufanikiwa kutoa msaada huo kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwauhalisia wanahitaji kutatuliwa changamoto ya Floraidi iliyozidi kwenye maji ya eneo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Jack amesema kuwa wamelazimika kutoa msaada huo baada ya kupata habari kupitia shirika la NASIO TRUST namna wananchi wa Lemanda walivyoathirika na madini ya Floraidi iliyozidi kwenye maji ya eneo hilo.
Amesema kuwa tumeona Floraidi ilivyoathiri wananchi wa eneo hilo hasa watoto ambao wamepata madhara kwenye mifupa na kusababisha kupinda miguu na kuona umuhimu wa kuchangia matanki hayo ili familia hizo zivune maji ya mvua yasiyo na madini ya Floraidi.
Nao wazee wa Kijiji cha Lemanda wamewashukiru wanafunzi hao na kuwaomba kiwasaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa kupata maji kutoka kwenye vyanzo vya maji ambavyo maji yake hayana madini ya Floraidi.
Hata hivyo licha ya msaada huo walioupata wananchi hao Mwenyekiti wa kitongoji cha Lemanda Ngavut Sivayo amemuomba Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha kuwasaidia kupata ufumbuzi wa kudumu kwa kuwa wamekuwa wakipata misaada ya kupunguza madini ya Floraidi kwenye maji ambayo ni utatuzi wa muda tuu.
" Haya matanki ni kweli yanatusaidia lakini tukuomba mkurugenzi sasa utufikirie tupate mradi wa maji yanayotoka kwenye chanzo cha maji yasiyo na kiasi kikubwa cha Floraidikwani wananchi wako tayari hata kuchangi upatikanaji wa maji safi na salama" amesema mwenyekiti huyo.
Wananchi wa kata ya Oldonyosambu na Oldonyowasi wameathirika na mdaini ya Floraidi yanayopatikana kwenye maji ya maeneo hayo yanayosababisha athari kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo ambao hupinda miguu na watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa, licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali kutoa msaada wa madini ya kupunguza kiasi cha Floraidi kwenye maji lakini bado ni changamoto kwa wakazi hao kununua mifupa hiyo pamoja na matumizi sahihi ya maji yaliyokingwa hasa kwa watoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments