Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekemea wazazi na walezi wanaowaficha watoto wenye ulemavu kwa kisingizio cha kuwaletea mikosi kwenye familia na kusema serikali haitawafumbia macho.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam kwenye kongamano la kwanza kitaifa la Urutubishaji wa chakula kwa mikoa ya Tanzania na kusema kuna baadhi ya wazazi wamekua wakiwanyima watoto wao haki ya msingi pindi wanapowabaini kuwa na ulemavu.
"Serikali haitalifumbia macho jambo suala la wazazi wanaoficha watoto wenye ulemavu na tutachukua hatua za haraka za kuwa nusuru watoto hao kwa kuwakamata walezi wao", alisema Mama Samia.
Pamoja na hayo, Makamu wa Rais amewataka watoa huduma za afya washirikiane na wataalam wa lishe ili waweze kuhakikisha wanaboresha huduma ya lishe kwa wazazi na kunusuru wajawazito kujifungua watoto wenye kasoro.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia , Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema wanasimamia sera ya afya kwa makini.
No comments:
Write comments