Thursday, August 17, 2017

Mikakati ya elimu yaimarika Arusha DC

Mwanafalsafa mkongwe nchini Italy Maria Montesory alizungumzia uhusiano wa mazingira bora na tendo la kujifunza kwa mwanafunzi na kueleza kuwa mazingira bora yenye kuvutia yanamwezesha mwanafunzi kuvutiwa na kujifunza kwa urahisi. Hayo yamejidhihirisha katika halamshauri ya arusha kwa kuwekeza zaidi kwenye ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari ili kuwa na mazingira bora yanayomuwezesha mwananfunzi kujifunza. Mwandishi wetu amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji halmashuri ya Arusha Dk. Wilson Mahera na mwandishi wetu na kueleza kuwa katika mwaka wa fedha uliosha wa 2016/2017 halmashauri imepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shuguli za maendeleo pamoja na kuwahudumia wananchi wa halmashauri hiyo Dk. Mahera amesema kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta karibu zote halmashauri ilijikita zaidi kuwekeza katika sekta ya elimu na tayari sekta hiyo imeanza kupata mafanikio kwa kiasi fulani tofauti na miaka iliyopita. Halmashuri imewekeza kiasi cha shilingi milioni 614 Fedha zilizotokana na fidia ya deni la shamba la Lakilaki kwa ajili kurekebisha miundombinu ya shule 62 za msingi na sekondari ikiwa ni pamoja ujenzi, umaliziaji na ukarabati wa madarasa, vyoo, maabara na nyumba za walimu. Kiasi cha shilingi milioni 420 kilitumika kuimarisha miundombinu ya shule 45 za msingi na shilingi milioni 194 kwenye shule 15 za sekondari ambapo mpaka sasa miradi hiyo imekamilika kwa zaidi ya asilimia 90% hali ambayo imeboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi wawapo shuleni. Mkurugenzi Mahera katika kuboresha sekta ya elimu halamshauri imefanikiwa kurekebisha na kusawazisha ikama ya walimu kwa kuwahamishia walimu kwenye shule za pembezoni ambazo zilikuwa na walimu wachache ukilinganisha na shule za mijini. “Hapo awali walimu walikuwa wamerundikana kwenye shule za mijini na shule za pembezoni kukosa walimu lakini hilo tumelitatua kwa kiasi kikubwa licha yakuwa zoezi hilo limetumia ghrama za uhamisho kwa walimu” amethibitsha mkurugenzi Aidha Dk. Mahera amesema kuwa kutokana na kuwa na zidio la walimu 273 wa masomo ya sanaa kwa shule za sekondari halmashuri pia imewapeleka walimu 70 kwenda kuongeza nguvu ya kufundisha katika shule za msingi. “Hii sio kuwafanyia demotion bali ni kusawazisha ikama ya walimu iendane na idadi ya wanafunzi na kwa kuwa sera ya elimu ya msingi kwa sasa ni kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne, na walimu wa shule za msingi wanatakiwa kuwa na kiwango cha elimu kuanzia stashahada na si cheti kama hapo awali”amesema Dk. Mahera. Halmashauri pia inatekeleza mpango wa kuhakikisha wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa kutekeleza mpango wa serikali maarufu kama KK tatu, mpango uliondoa mzigo wa masoma kwa madarasa hayo na kubakiza masomo ya Kusoma, kuandika na kuhesabu peke yake. Tunasimamia ufundishaji wa KK tatu katika madarasa ya awali la kwanza na la pili kwa kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo kwa kutumiza zana zinapatikana kwenye mazingira husika na kuwapima wanafunzi hao kabla ya kupanda darasa. “Kwa sasa tuna walimu maalumu wa kufundisha madarasa hayo na wamepatiwa mafunzo maalumu ya mbinu za ufundishaji KK tatu na walimu hao ni wakudumu katika shule hawatahamishwa katika shule hizo bila sababu maalum ili kuhakikisha mpango huo unafanikiwa” amesisistiza Mwalimu wa anayefundisha darasa la kwanza na la pili shule ya msingi Olchoki mwalimu Asnath David amethibitisha uwepo wa mkakati thabiti wa kuhakikisha mwanafunzi anapoingia darasa la tatu anjua kusoma ,kuandika na kuhesabu hili litaondoa tatizo la wanafunzi kumaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika. “Utaratibu wa sasa wa kufundisha masoma matatu kwa mwanafunzi wa madarasa haya unawapunguzia watoto mzigo wa masomo na kuwawezesha kujifunza haraka na kwa urahisi stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu tofauti na miaka ya hivi karibuni wanafunzi hao walipokuwa wanaanza shule na kusoma masomo mengi” amesema mwalimu David Dk. Mahera ameenda mbali zaidi na kusema kuwa katika shule za sekondari tuna walimu wa ziada wa masomo ya sanaa hivyo tumejikita katika kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwa kuanza kuondoa alama sifuri kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata alama D kwenye masomo ya Sanaa. “Tumejipanga kuondoa zero kwa wanafunzi wa form four kwa kuhakikisha mwanafunzi anapata alama D kwa masomo ya Historia, Kiswahili, Jiografia na English na inawezekana kutokana na idadi kubwa ya walimu wa masomo hayo. “Kwa hili tutawapima walimu kutokana na ufaulu wa wanafunzi na si kwa kumaliza sylubus peke yake, niko serious na hili kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa shule za sekondari” amesisistiza Dk. Mahera Afisa Elimu Taaluma elimu Sekondari mwalimu John Charle amethibitisha kutumika kwa mkakati wa kuondoa alama sifuri kwa wanafunzi wa kidato cha nne kwa kuwakufundisha wanafunzi wa madarasa ya mitihani kwa muda wa ziada ambapo hufanyika asubuhi kabla ya vipindi na jioni baada ya vipindi kwa kufanya marudio na mazoezi mengi ya maswali ya mitihani. “Kwa sasa tunasimamia mkakati huu na walimu na wanafunzi wameshajitune kwa pamoja kuhakikisha tunaondoa sifuri katika shule zetu” amesema Charles. Ameongeza kuwa tayari majaribio ya mkakati huu umeanza kuonyesha mafanikio kwa matokeo ya mtihani ya ndani pamoja na mtihani wa udhamiri halmashuri yetu imeshika nafasi ya kwanza kwa mkoa wa Arusha na tunategemea kufanya vizuri hata katika mtihani wa taifa. Hata hivyo Dk Mahera amethibitisha kuwa na upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na kusema kuwa serikali sasa imeweka kipaumbele cha kuajiri walimu wa masomo hayo zaidi na pia shule zetu zina maabara za sayansi kwa asilimia zaidi ya 90%. Mkurugenzi Mahera ameweka wazi kuwa mkakati wa uboreshaji sekta ya elimu unakabiliwa na changamoto kubwa ya nyumba za kuishi walimu hasa katika shule za pembezoni ambazo hakuna nyumba za wenyeji ambazo walimu wangeweza kupanga na kuishi huko jambo linalosababisha adha kubwa kwa walimuya usafiri wa kufika shuleni. “Walimu wa pembezoni wanakapata adha kubwa ya gharama kubwa ya nauli ya kwenda na kurudi shuleni mwalimu anaweza kutumia nauli ya mpaka shilingi elfu nane kwa siku ambayo ni gharama kubwa kwa mtumishi wa umma” amesema Dk. Mahera Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema halmashauri inahitaji nyumba zaidi ya 2500 ili kuondoa tatizo hilo ambazo zitagharimu takribani bilioni 900 ambapo halmashauri imeanza kufikiria kutafuta mwekezaji atakaewekeza kwenye ujenzi wa nyumba hizo kwa kufanya hivyo tatizo hilo linaweza kumalizika kwa kuwa serikali haina uwezo wa kujenga nyumba hizo. Mkurugenzi Mahera anawataka wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza kuwekeza na kuchangia shughuli za maendeleo katika halmshauri ya Arusha ili kuhakikisha Tanzania inafikia malengo ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020/2025.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo