Ujenzi na Upanuzi wa miundo mbinu ya Kituo cha Afya Nduruma halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru unaendelea vizuri miezi miwili baada ya halmashauri kupokea fedha kiasi cha Shilingi milioni 500 kutoka Serikali kuu.
Fedha hizo zimetolewa na Serikali kwa lengo la kuhakikisha kituo hicho kinakuwa na hadhi ya Nyota tano na kutimiza adhma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha Afya chenye hadhi hiyo.
Kiasi hicho cha fedha kinatumika kujenga majengo mbalimbali ikiwemo jengo la Maabara kwa ajili ya vipimo, jengo la Mama na Mtoto 'Maternity Ward', jengo la kuhifadhia Maiti 'Mortuary', jengo la kuchomea taka 'Incinerator', nyumba ya Mganga pamoja na umaliziaji wa jengo la upasuaji 'Operation Theater'.
Hata hivyo ili kuhakikisha fedha hizo zinakamilisha ujenzi huo kwa wakati na kwa gharama nafuu, Halmashauri imelazimika kutumia Mafundi wa kawaida 'local fundi' badaya kutumia Mkandarasi njia inayojulikana kama 'Forced Account' kulingana na kanuni na taratibu za manunuzi ya Serikali.
Kituo hicho cha Afya kinategemea kuhudumia wananchi wa kata ya Nduruma na kata za jirani za Bwawani, Mlangarini na baadhi ya maeneo ya Jiji la Arusha.
![]() |
Jengo la kuhifadhia Maiti 'Mortuary' |
![]() |
Nyumba ya Daktari |
![]() |
Jengo la Mana na Mtoto 'Maternity Ward' |
![]() |
Jengo la Maabara |
No comments:
Write comments