Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa orodha ya wanafunzi waliyoomba mkopo wa elimu ya juu kwa mwaka wa fedha 2017/2018 baada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo.
o ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018, orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo imekamilika.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Mikopo Abdul-Razaq Badru katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumatano Oktoba 18,2017 amesema kuwa jumla ya wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo na jumla ya Shilingi bilioni 34.6 zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao.
Amesema kuwa awamu nyingine itatolewa kwa jumla ya wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza itakayogharimu jumla ya Shilingi bilioni 108.8.
Bandru ametihibitisha kuwa orodha ya majina ya awamu ya kwanza inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo http://www.heslb.go.tz/ na itatumwa kwa vyuo husika.
Aidha Bandru amefafanua kuwa orodha nyingine (batches) zitafuata kwa kadri utaratibu wa udahili na uchambuzi utakavyoendelea kukamilika.
“Lengo ni kutoa majina ya wote waliofanikiwa kupata mkopo kabla ya vyuo kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba, 2017,” amesema.
Mkurugenzi mtendaji huyo amesema orodha hiyo ya wanafunzi 10,196 imepatikana baada ya kupokea na kuchambua awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495 waliopata udahili katika chuo kimoja.
“Itakumbukwa kuwa moja ya sifa kuu za kupata mkopo ni mwombaji kupata udahili katika taasisi ya elimu ya juu inayotambuliwa na Serikali,” amesema.
Amesema wanafunzi waliopata udahili katika chuo zaidi ya kimoja na ambao wana sifa za kupata mikopo, watapangiwa mikopo baada ya kuchagua na kuthibitisha chuo watakachojiunga kwa ajili ya masomo.
Wakati huohuo, Badru amesema wanatarajia kuanza kutuma vyuoni fedha za mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wamefaulu mitihani yao kuanzia leo Jumatano, Oktoba 18, 2017.
Amesema Sh318.6 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2017/2018.
“Tayari Serikali imeshatoa fedha hizo na lengo la Bodi ni kuhakikisha zinafika vyuoni kabla ya kufunguliwa kwa vyuo ili kuwaondolea wanafunzi usumbufu,” amesema.
Bodi imewasihi waombaji wa mikopo kuwa na subira wakati ikiendelea kukamilisha maandalizi ya orodha zinazofuata za wanafunzi waliopata mikopo.
No comments:
Write comments