Watu watatu wamekufa maji huku wawili wakinusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama walipokuwa wakijirabu kuvuta mto Ruvu wakitokea Vigwaza kwenda Mlandizi mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Jonathan Shana amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali hiyo imetokea Jumamosi asubuhi kwenye Mto Ruvu wilayani Chalinze na kusababisha vifo vya watu watatub,huku waili wakinusurika licha ya kuwa nahodha wa mtumbwi huo hajulikani alipo.
Kamanda Shana amesema kuwa ajali hiyo imepoteza maisha ya watoto wawili ambao ni Nusrat Haji miezi minne na Feisal Hamza mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu pamoja na Sikuzani Musa (41), ambaye mwili wake bado haujapatikana.
Kamanda Shana aliwataja walionusurika ni Zuwena Ramadhan (29) na Tero Mziray (20) ambapo dereva wa mtumbwi huo hajulikani alipo na inaaminika hakufa maji.
“Chanzo cha mtumbwi huo kuzama bado kinachunguzwa na miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi,” aliongeza.
Hata hivyo Kamanda huyo amewataka wamiliki wa vyombo hivyo kuhakikisha vinakuwa kwenye hali nzuri ili kuepukana na ajali kama hizo ambazo zinapoteza uhai wa watu kutokana na ubovu.
No comments:
Write comments