Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefanya marekebisho katika Ngao ya Jamii ambayo timu ya Simba ilikabidhiwa baada ya kuifunga Yanga siku ya Jumatano ya wiki iliyopita.
Awali Ngao hiyo ilikosewa katika kuandika neno SHIELD na kuandikwa SHELD Simba walikabidhiwa lakini baada ya makosa kuonekana TFF waliomba radhi siku iliyofuata kisha kuwaambia Simba wairejeshe Ngao hiyo kwa ajili ya marekebisho ya neno hilo.
Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas ameionyesha Ngao iliyorekebishwa kwa waandishi wa habari leo Jumanne kwenye ofisi za shirikisho hilo Karume jijini Dar.
No comments:
Write comments