Sunday, August 6, 2017

Rais Magufuli agoma kumsamehe mwekezaji kodi anayodaiwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekataa ombi la kumsamehe kodi mwekezaji wa kiwanda cha saruji cha Kilimanjaro kilichopo mkoani Tanga.

Rais Magufuli amekataa ombi la msamaha wa kodi wanayodaiwa kwa muda wa miaka 10 walipowasilisha waliposoma risala ya kiwanda hicho na kueleza kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Rais Magufuli ametoa msimamo huo wakati akitoa hotuba  katika hafla ya uzinduzi na  kujibu maombi yaliyokuwa katika risala ya kiwanda hicho, ambacho kilitaka kisamehewe kodi wanayodaiwa kwa muda wa miaka 10 kutokana na deni kubwa ambalo kiwanda hicho  kinadaiwa katika taasisi za kifedha, zilizokopwa kama mtaji wa kukianzisha.

Risala hiyo ilieleza sababu nyingine za kutaka kiwanda hicho kusamehewe kodi ni kutokana na mchango wake katika shughuli za kijamii ikiwemo kuchangia madawati na vyumba vya madarasa katika shule za jiji hilo pamoja na kusaidia huduma za maji.

Hata hivyo Rais Magufuli amesisitiza kuwa haiwezekani kufanya uamuzi wa kusamehe kodi na kuikosesha serikali mapato na kuongeza kuwa serikali yake inahimiza viwanda ili iweze kupata mapato kupitia kodi zitakazolipwa na viwanda hivyo.

"Nianze kumshukuru rmwenye kiwanda kwa kutoa misaada kwa jamii, na kwa vile mifuko ya saruji 1300 aliyoitoa nilikuwa hapa nikija nitataka mnipeleke sehemu zilipotumika. Lakini uliniomba kusamehe kodi hilo ni ombi gumu.

Wito wa serikali kuhimiza kujenga viwanda maana yake ni kwamba serikali ipate pesa tuweze kusomesha watoto bure, kuongeza madawa hospital nk, ninachokuomba ni wewe tu ujipange ndiyo ushindani wenyewe"amesisitiza Rais

Katika hatua nyingine, rais Magufuli ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na wazawa kwa hatua hiyo ya kufanya uzalishaji na kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 100

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...