Sunday, August 6, 2017

Kampeni za Uchaguzi Mkuu Kenya zahitimishwa rasmi jana

Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Kenya unaotarajiwa kufanyika siku ya  Jumanne tarehe 08.08.2017 ya wiki ijayo zimehitimishwa hapo jana kwa vinara wawili wagombea Urais wanaopewa nafasi kubwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kuhitimisha kampeni zao kwa kuwataka wananchi kuwa watulivu na kudumisha amani.

Akifunga kampeni hizo Mgombea wa Jubilee na rais wa sasa nchini Kenya Uhuru Kenyatta amehitimisha kwa kuahidi elimu bure kwa wakenya wote kuanzia shule ya msinhi hadi sekondari pamoja na kukamilisha miradi ambayo tayari serikali iliyoko madarakani imeianzisha.

Naye kiongozi wa muungano wa Upinzani NASA Raila Odinga amewataka wapiga kura kujitokeza kwa wingi kumpigia kura na kuahidi kuwa akiingia madarakani ataondoa rushwa ambayo anasema mpinzani wake Uhuru Kenyatta ameshindwa kuiondoa.

Uchaguzi huo wa Kenya unaoangaziwa sana kutokana na mvutano wa kisiasa uliopo baina ya wagombea wawili wanaopewa nafasi kubwa unatarajia kuwa wa amani licha ya wasiwasi uliojitokeza kufuatia kifo cha mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Chriss Msando.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...