Thursday, November 30, 2017

Maadhimisho ya siku ya UKIMWI DUNIANI kufanyika kwenye Soko la Kisongo Halmashauri ya Arusha




Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera anawatangazia wananchi wote wakazi wa Halmashauri ya Arusha kuhudhuria kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI DUNIANI yatakayofanyika kesho tarehe 01/12/2017 kwenye Viwanja vya Soko la Kisongo kata ya Matevesi.

Maadhimisho hayo yataambatana na Upimaji wa virusi vya UKIMWI na utoaji Ushauri Nasaha pamoja Uchangiaji wa MFUKO WA KUDHIBITI UKIMWI.

Kauli Mbiu ya siku ya UKIMWI DUNIANI:

"CHANGIA MFUKO WA UDHAMINI WA KUDHIBITI  UKIMWI NCHINI UOKOE MAISHA"

Wananchi wanatakiwa kuchangia kupitia Simu zao za mkononi kupitia namba  0684 909090.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...