Monday, August 14, 2017

Watumishi wa halmashauri ya Arusha watakiwa kufanyakazi kwa weledi

Watumishi wa halmashauri ya Arusha wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, uaminifu, uzalendo pamoja na kuzifuata kanuni, sheria na miongozi ya serikali kwa kufanya hivyo kutaleta chachu ya maendeleo katika halmashauri hiyo. Akizungunza na watumishi hao katika ukumbi wa Green Acres Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Dk. Wilson Mahera amewataka watumishi hao kufanyakazi kwa kujituma kutokana na taaluma zao walizoajiriwa nazo. Hata hivyo Dk. Mahera amewapongeza watumishi kwa kufanya kazi kwa bidii mwaka uliopita na hilo limedhihirisha kuwa watumishi wapo tayari kwa mabadiliko ya kuitumikia serikali na wananchi kwa ujumla ambao ndio waajiri wao. "Ninafurahishwa na watumishi wengi kuonekana kubadilika kuendana na kasi ya maendeleo, ninachohitaji ni kila mtu afanye kazi kwa uhuru bila woga ila kwa kufuata sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma" amesisitiza Dk. Mahera Aidha Mkurugenzi huyo amewataka watumishi kuwa na mpango kazi wa kila siku ambao utaendana na mpango mkakati wa halmashauri na kufanya tathmini ya utekelezaji wake kila siku baada ya kazi hii itamuwezesha mtumishi kufikia malengo ya utendaji kazi wake. Pia amewataka watumishi kutumia taaluma zao kiandika maandiko ya miradi ambayo itaisaidia halmashauri kupata wafadili watakaowekeza kwenye miradi ya maendeleo itakayosaidia kutatua changamoto za huduma za jamii ndani ya hamashauri. Licha ya changamoto ya upungufu wa rasilimali lakini watumidhi wanatakiwa kuwa wazalendo wa kujitolea kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia raslimali chache zilizopo. Akizungumza kwa niaba ya watumishi, Afisa Utumishi ndugu Abihud Mwakijambile amesema kuwa tangu Mkurugenzi alipoteuliwa na mheshimwa Rais kuwa kuiongoza halmashauri hii kumekuwa na mabadiliko ya wazi ya kiutendaji ambapo sasa kila mtumishi anajituma kulingana na taaluma yake. "Kwa sasa watumishi wanawajibika bila kusukumwa kumekuwa na mwamko mkubwa za watumishi kufanya kazi licha ya changamoto zinazowakabili tofauti na vipundi vya nyuma" amesema Abuhudi. Mkurugenzi huyo amefanya kikao na watumishi wa Makao Makuu halmashauri ya Arusha kwa lengo la kukumbushana masuala ya utendaji na uwajibikaji ili kufikia malengo ya Mpango zmkakati wa miaka 10 wa halmashauri ya Arusha.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo
Loading...