Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzanua Dk. John Pombe Magufuli ametoa oda ya kuhaisha ujenzi wa uwanja na kituo cha michezo uliopangwa kujengwa eneo la Nara nje kidogo ya mji wa Dodoma na badala yake ujenzi huo ufanyike maeneo yaliyo karibu ma mji wa Dodoma.
Awali eneo la kujenga uwanja huo lilitolewa naMamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Dodoma iliyotenga Ekari 143 zilizopo Nara Barabara ya Singida nje kidogo ya mji wa Dodoma kitakachojengwa kwa msaada wa serikali ya Morocco.
Waziri wa Habari Dk, Harrison Mwakyembe amesema kuwa Rais Magufuli alitoa oda ya ujenzi wa uwanja huo kuhamishwa na kupelekwa maeneo yaliyo karibu na mji wa Dodoma ili kutoa fursa kwa vijana na watoto kutumia uwanja huo pindi utakapokamilika kwani sehemu ambayo ilitengwa awali ni mbali sana kutoka mjini Dodoma.
"Tunamshukuru sana Rais wetu wa Tanzania Magufuli kwa kuikumbuka sekta ya michezo kwa kuomba Morrocco watujengee eneo changamani, walio wengi wanafikiri ni kiwanja cha mpira wa miguu lakini hapana hili ni eneo changamani litakuwa na michezo ya aina yote, mwanzoni kama mnakumbuka tulipata eneo Nara eneo kubwa tu tuliomba ekari 150 tulipewa lakini Mhe. Rais Magufuli aliona kuna umbali kutoka Dodoma mjini mpaka Nara zaidi ya kilomita 70 akaona siyo rafiki, yeye angependa kuona vijana wake wa shule ya msingi na sekondari wakitoka shule wanakimbia uwanjani na umbali usiwe kikwazo" alisema Mwakyembe
Aidha Mwakyembe anadai kuwa Rais Magufuli aliagiza litafutwe eneo lingine
"Rais Magufuli aliagiza litafutwe eneo karibu na Dodoma mjini tujenge hiyo 'stadium' na kwa bahati nzuri sana agizo la Rais lilitekelezwa, tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha tunapata eneo zuri kuelekea Dar es Salaam karibu na Nane Nane linaitwa Zuguni ambapo sasa tumepata ekari 300 na hizo zote tunazihitaji kwa sababu tunataka eneo hili changamani liwe la mfano katika ujenzi wa viwanja Tanzania kwa sababu tunataka baadaye kuwa na hoteli, kuwe na hosteli kwa vijana, tuwe na majumba makubwa ya michezo" alisisitiza Mwakyembe
Wahandisi, wabunifu na wataalam wa udongo kutoka nchini Morocco wameingia nchini Tanzania kufanya ziara na tathmini juu ya ujenzi wa eneo hilo changamani Dodoma
No comments:
Write comments