Thursday, August 17, 2017

Boniface Mkwasa afunguka kupigwa mnada jengo la Yanga


Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga  Charles Boniface Mkwasa amekiri klabu hiyo kudaiwa kodi na serikali na kuwataka mashabiki na wanachama wa Yanga kuwa watulivu katika kipindi hiki.

Mkwasa amebainisha hayo  baada ya taarifa hizo kuwepo kwenye vyombo vya habari kuhusu jengo lao kupigwa mnada siku ya Jumamosi

“Ni kweli tuna deni kubwa tunadaiwa na ardhi lakini tayari tulifanya nao mazungumzo na kukubaliana namna ya kulilipa kupitia mapato yetu ya milangoni. Tunategemea kuanza kuendelea kulipa baada ya ligi kuanza  hivi karibuni, tutatoa taarifa rasmi baadaye”, alisema Mkwasa.

Mkwasa amesema kiasi wanachodaiwa ni kikubwa lakini hakizidi shilingi milioni 500, huku akiweka wazi kuwa pesa wanayotakiwa kulipa kwa mwaka ni shilingi milioni 59.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia kwa kampuni ya udalali ya Msolopa Investmenst Limited leo imetangaza kulipiga mnada jengo hilo endapo Yanga hawatalipa kabla ya Agosti 19, mwaka huu.

No comments:
Write comments

Matangazo

Matangazo